JUMLA YA MITI 132 YAOTESHWA KATA YA IBISABAGENI WILAYANI SENGEREMA
Jumla ya miche mia moja
thelathni na mbili(132) ya miti imepandwa kwenye eneo la stendi ya mtaa wa Ibisabageni kata ya Ibisabageni
wilayani Sengerema kwa lengo la kuenzi kauli ya kuboresha mazingira kwa nchi nzima.
Miche hiyo imepandwa katika uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika katika kata ya Ibisabageni wilayani hapa ambapo Zoezi
hilo limeongonzwa na mkuu wa wilaya ya Sengerema
Mh. EMMANUEL ENOCK KIPOLE.
Mh. Kipole
amewapongeza wananchi wa mtaa huo kwa
kuonyesha jitihada kubwa za kuchangia
pesa kiasi cha shilingi mia mbili kwa
kila mwananchi kwa ajili ya upatikanaji
wa miti hiyo.
Kwa upande wao baadhii ya wananchi wa mtaa huo wamemshukuru
mkuu wa Wilaya kwa kuzindua zoezi hilo kwani miti ni muhimu katika kutunza mazingira .
Sanjari na hayo mkuu
huyo wa wilaya amewaagiza mwenyekiti wa mtaa
pamoja na Afisa mtendaji
wa kata hiyo kuwa
mstari wa mbele kuimarisha ulinzi wa
rasilimali hizo ili
zisiharibiwe na mifugo .
Na Esther Mabula
Comments
Post a Comment