HUDUMA YA MAJI YATARAJIWA KUREJESHWA SAA TANO USIKU FEB 08 WILAYANI SENGEREMA

Huduma ya maji Wilayani Sengerema Mkoani
Mwanza inatarajiwa kurejea katika hali yake ya kawaida usiku wa leo majira ya saa tano na kumaliza usumbufu kwa wananchi wa kusaka maji umbali mrefu na kutumia maji ya kwenye mifereji yasiyo safi
na Salama.
Neema hiyo imetangazwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halamsahauri ya Wilaya
ya Sengerema Bwn, Magessa Mafuru
Boniphace wakati akizungumza na Radio Sengerema kwa njia ya simu akiwa Mjini Dodoma
ambapo amesema
kuwa
wakazi wa Sengerema wasubiri neema hiyo
usiku wa leo huduma hiyo muhimu kwa shauku kubwa na kwamba kwa sasa katika chanzo cha maji cha
Nyamazugo Wilayani Sebngerema wameanza kuruhusu maji
kwa ajili ya kujaza matenki ya maji na kisha usiku watayaruhusu ili yawafikia wananchi.
Aidha Bwn, Boniphace
katika kutambua umuhimu wa wananchi wa halmashauri yake amewaomba radhi kwa
usumbufu walioupata kwa siku 24 toka
lilipotokea katizo la maji katika mji wa Sengerema huku akiwaomba wananchi waendelee kulipa bili ya
jai kuepusha kujitokeza tena katizo hilo la maji mara kwa mara .


Comments
Post a Comment