ZAIDI YA KAYA 250 KATI YA 500 HAZINA VYOO KITONGOJI CHA MSIKITINI HALMASHAURI YA BUCHOSA
Zaidi ya kaya 250 kati ya 500 hazina vyoo katika kitongoji cha Msikitini kilichopo katika kijiji cha Kanyara
kata ya Bulyaheke Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema Mkoani Mwanza.
Akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara Mwenyekiti wa kitongoji hicho Samola Makubi amesema kaya nyingi zina kabiliwa na ukosefu wa vyoo
ambapo kati ya kaya 5 kaya 3 zimekuwa hazina vyoo hali ambayo hulazimu
kujisaidia ovyo.
Kufuatia hali hiyo
Mwenyekiti huyo imemlazimu kutoa siku 6 kwa
kaya hizo kuhakikisha zinakuwa na
vyoo vyinginevyo msako mkali utaanza kwa wale watakao kaidi agizo hilo.
Baada ya mkutano huo
kuahirishwa wananchi wakaunga mkono agizo la mwenyekiti huyo.
Kitongoji cha Msikitini
licha ya kukabiliwa na ukosefu wa vyoo lakini ni miongoni mwa vitongoji vikubwa
vilivyoko katika kijiji cha Kanyara ambacho
kina kadiliwa kuwa na kaya 500 na jumla ya wakaazi wapatao alfu nane (8000)
hali ambayo hulazimu kujisaidia kwa kuchangia vyoo kwa kaya jirani wengine
wakilazimika kutumia mifuko ya lambo kujisaidia huku wengine wakijisaidia
katika fukwe za ziwa Victoria.
KATEMI LENATUS.
Comments
Post a Comment