WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI ISACK KAMWELE AMUBADILIKIA MHANDISI WA MAJI MKOA WA MWANZA ATAKA UKWELI JUU YA KUTOKAMILIKA KWA MRADI WA MAJI BUCHOSA.
Waziri
wa maji na umwagiliaji Eng, Isack Kamwele amemuagiza mhandisi wa maji mkoa wa
mwanza kupeleka watalamu katika miradi ya maji iliyopo katika halmashauri ya
Buchosa ilikubaini sababu zinazo pelekea miradi hiyo kuto kukamilika kwa
wakati.
Eng, Kamwele ametoa agizo hilo baada ya
kutembelea mradi wa maji wa luchili na Lumeya ambapo amebaini miradi hiyo hadi
sasa imekwisha tumia asilimia 5 ya fedha huku fedha zingine zikiwa
hazijatumika.
Hata hivyo ameshangazwa na utata uliopo kwa
halmashauri za Sengerema na buchosa kushindwa kuweka wazi makabidhiano ya
miradi hiyo ambapo halmashauri ya buchosa imedai kuto kabidhiwa
miradi kutoka halmashauri ya Sengerema ili hali halmashauri ya Sengerema
ikikili kukabidhi miradi hiyo katika halmashauri ya buchosa.
Awali akikagua miradi hiyo ameipongeza
halmashauri ya Sengerema kwa kukamilisha mradi wa maji wa Nyamazugo kwa
asilimia 100,ambapo amesema amefurahishwa na hatua hiyo kwani tayari wananchi
wa Sengerema wananufaika na mradi huo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Sengerema Mh Emmanuel Kipole amemhakikishia waziri wa maji kuhakikisha anachukua hatua kwa mkurugenzi atakaye baina kuidanganya ofisi ya mkuu wa wilaya, kuwa tayari makabidhiano yalishaa fanyika kwa halmashauri hizo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha
mapinduzi ccm wilaya ya Sengerema Bwana Mac Agustine Makoye ameitaka serikali
kuchukua hatua za haraka kubaini ugumu wa kuto kukabidhiana miradi kwa
halmashauri hizo kwani kufanya hivyo ni kukwamisha ilani ya ccm ya mwaka 2015.
Na Katemi Lenatus.
Comments
Post a Comment