WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AKABIDHI SH,MILION 20 KWA AJILI YA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI
Waziri
wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack
Kamwele amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 20 kwa ajili ya mradi wa
maji katika mtaa wa Bukala kata ya
Ibisabageni wilayani Sengerema mkoani
Mwanza.
Akizungumza
katika mkutano wa wananchi na viongozi wakati akikabidhi mabomba hayo , katika mtaa
wa Bukala amesema kuwa wananchi
washirikiane pamoja na viongozi ili kuweza kupata maji safi na salaama na kutoa
agizo kuwa ndani ya wiki tatu maji yawe
yamepatikana.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Sengerema
mh.Emmanuel Kipole amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutumia nguvu kazi
ili kuhakikisha zoezi la upatikanaji wa
maji linakamilika mapema na kuondokana na changamoto hiyo .

Mh
.kipole ameongeza kwa kusema kuwa wanafanya jitihada za upatikanaji wa maji
katika maeneo mbalimbali ili kusaidia wananchi na kuunga mkono kauli ya mh.
Rais wa awamu ya tano Dkt .John Pombe Magufuli ya kumtua ndoo ya maji mama.
Pia
wananchi wamemshukuru waziri wa maji na
umwagiliaji mhandisi kamwele na kusema kuwa, tatizo la maji limekuwa
likiwasumbua kwa muda mrefu hivyo wamepokea mabomba hayo kwa furaha .
Na Glorius Balele.



Comments
Post a Comment