WANANCHI WAHIMIZWA KUTUNZA MAHINDI WALIYOYAVUNA ILI KUJIKIGA NA BAA LA NJAA WILAYANI SENGEREMA
Wananchi wa
mtaa wa Kilabela kata
ya Mwabaluhi wilaya
ya Sengerema, Mkoani Mwanza
wametakiwa kutunza Mahindi
Waliyoanza kuyavuna kwenye
mashamba yao ili kujikinga na baa la njaa katika siku za
usoni.

Akizungumza na
Redio Sengerema Ofisini
kwake januari 5 mwaka
huu, mwenyekiti wa mtaa
huo Bwn, Samweli
Macheni Nzungu, amekemea
kitendo cha wananchi
kusahau shida ya uhaba wa
chakula iliyokuwa ikiwakabili na
badala yake wameanza
kuuza chakula, hali
ambayo bila kuikomesha kwa
sasa huenda ikasababisha njaa
hapo badae.
Mwenyekiti
Nzungu amesikitishwa
na kitendo cha baadhi ya wananchi
kuuza chakula na
kusema kuwa, wananchi
wanatakiwa kukumbuka hali
waliyokuwa nayo hapo awali ,huku
akionya mtu yeyote
atakayeonekana na mahindi
mabichi akamatwe na
uchunguzi ufanyike ikiwemo
kuonana na alieuza
mahindi hayo kwa hatua
zaidi za kisheria.
Aidha Bwn ,Macheni
amelaani vikali kitendo
cha
kukata mahindi mabichi
na kwenda kuuza
kwa wachomaji, na kuwataka waache
tabia hiyo, kwa madai kuwa
hali hiyo inaweza
kusababisha watu kuibiwa
mahindi yao pamoja
na kumaliza mahindi yakiwa mashambani
na kujutia baadae.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment