WANANCHI WA MTAA WA IBISABAGENI SENGEREMA WAADHIMIA KUPANDA MITI
Mwenyekiti wa
mtaa wa Ibisabageni
kata ya Ibisabageni
wilayani Sengerema,
ameadhimia kuboresha mazingira
kwa kupanda miti
mtaani hapo ili
kuunga mkono kampeni
ya serikali
ya kutunza mazingira nchini.

Hayo yamebainishwa
na mwenyekiti wa
mtaa huo Bwn,
Stanle Felix, katika
kikao cha hadhara
mtaani hapo, chenye
lengo la
mipango mikakati
ya maendeleo ya mtaa huo kwa
mwaka 2018.
Hata hivyo Bwn,
Felix amesema kuwa
kuwa jukumu
la kuchangisha michango yoyote ya maendeleo
kwa
wapangaji libaki kwa wamiliki
wa nyumba sambamba
na kumuunga mkono
kwa ajili ya upandaji miti,
na ujenzi wa
ofisi ya mtaa.
Kwa
upande wao wananchi katika kikao
hicho wameibua
baadhi ya kero kwa baadhi
ya wapangaji ikiwemo kutotoa michango
pindi inapohitajika kuchangia
katika maendeleo
ya mtaa huo.
Katika hatua
nyingine mwenyekiti huyo
amewahakikishia wananchi wake kuwa maendeleo
hayaji bila kuwa
na mipangilio na mipango mahususi, ikiwa ni
pamoja na Machungu
ya kufanya kazi
kwa bidii.
Na Thobias Ngubila.
Comments
Post a Comment