WAANDISHI WA HABARI 5 WAWEKWA NDANI KWA KUJIFANYA MAAFISA USALAMA WA TAIFA
Waandishi wa habari watano wilayani Kahama mkoani Shinyanga
wamefikishwa mahakamani wilayani Kahama kwa makosa ya kujifanya maafisa usalama
wa taifa kutoka ikulu na kujipatia fedha shilingi Milioni 1 kutoka kwa mganga
wa jadi Jane Mbeshi (46).

Waandishi wa habari wanne kati ya watano ambao ni Paul
Kayanda wa gazeti la Uhuru,Raymond Mihayo- Habarileo,Shaban Njia – Jamboleo,Simon
Dioniz – Radio Kwizera wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kahama
Jumatano Januari 10,2018 na George Maziku ambaye hajulikani anaandikia chombo
gani anatafutwa.
Akisoma mashtaka mahakamani hapo Hakimu Kazi wa mahakama ya
wilaya ya Kahama,Keneth Mutembei amesema
washtakiwa hao wamejifanya maafisa wa usalama wa taifa kutoka Dar es
salaam,Kigoma,Kagera,Shinyanga na Kahama kisha kujipatia shilingi Milion (1,000,000)/-
kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi
(46) mkazi wa kitongoji cha Ng’wande kata
ya Mwaluguli wilayani Kahama baada ya kumtishia kuwa anapiga
ramli chonganishi.
Amesema waandishi wa habari watatu ambao ni Paul Kayanda,Shaban Njia na Dioniz Maziku wamekamatwa Januari 9,2018 saa saba na nusu mchana na jeshi la polisi wakijifanya maafisa wa usalama wa taifa na kujipatia fedha kutoka kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi.
Mara baada ya kusoma mashtaka hayo,hakimu huyo alisema
dhamana ipo wazi kwa washtakiwa ambapo walikana mashtaka hayo walikana kutenda
makosa hayo.
Washtakiwa walirudishwa gerezani baada ya kushindwa kutimiza
masharti ya dhamana.
Comments
Post a Comment