VICHAKA VYAGEUKA KUWA VYOO KATIKA MNADA WA MIFUGO WA KAMENA MKOANI GEITA
Wananchi wanaopeleka mifugo yao kuuza katika Mnada
wa Kamena uliopo katika kata ya Kamena Mkoani Geita wanalazimika kujihifadhi kwenye vichaka kutokana na mnada huo kukabiliwa na ukosefu
wa choo kwa zaidi ya mika 43 bila
kupatiwa ufumbuzi.
Radio Sengerema imezulu
katika mnada huo na kujionea idadi kubwa
ya wananchi wamegeuza vichaka kuwa choo
hali ambayo itasababisha wananchi hao
kukumbwa na magonjwa ya mlipuko katika
kipindi hiki cha mvua zinazoendelea
kunyesha.
Licha ya mnada huo kuingiza mapato mengi katika halmashauri
ya Geita lakini hadi sasa hakuna huduma
ya choo katika mnada huo.
Diwani wa kata ya Kamena Mh,Peter Kulwa alipotafutwa na Radio Sengerema kwa njia ya simu amekata simu kwa
madai kuwa yupo kwenye kikao hawezi
kulizungumzia jambo hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya
Geita All Kidwaka ameahidi kulishughulikia suala la
ujenzi wa huduma
ya choo katika mnada huo haraka
iliwezekanavyo ili kunusuru wananchi kujihifadhi kwenye vichaka.
Na Emmanuel Twimanye.



Comments
Post a Comment