UPUNGUFU WA VIFAA WASABABISHA KUKWAMA ZOEZI LA UPIMAJI VIWANJA SENGEREMA
Upungufu wa
vifaa umepelekea zoezi la upimaji wa viwanja kuchelewa
katika mtaa wa Kanyamwanza
kata ya Mwabaluhi
wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza.

Akizungumza katibu
wa kamati ya
upimaji na urasimishaji
wa viwanja katika
mtaa huo Bwn,Joseph Maxmilian Kayanda ameeleza upimaji
ulivyoanza mtaani hapo.
Katibu huyo
amezungumzia jitihada wanazozifanya
kama kamati kuhakikisha
kampuni ya Geop
Geomatic Interprisess inaongeza
vifaa ili kukamilisha upimaji kwa
wakati.
Hata hivyo
Bwn, kayanda amekiri
kukumbana na changamoto
katika zoezi hilo
ikiwemo uelewa mdogo wa wananchi
juu ya
hatimiliki inayatolewa sasa
na Ofa zilizokuwa zikitolewa
awali.
Aidha katibu huyo
amewataka wananchi kutambua
umuhimu wa hatimiliki
na kwamba inaweza
kuwasaidia katika mambo mbalimbali sambamba
na kuwa na
uhakika wa kumiliki
aridhi kisheria.
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment