UKOSEFU WA ELIMU YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UMESABABISHA WANANCHI KUVAMIA MAPORI YA AKIBA MKOANI KAGERA
Ukosefu
wa elimu juu ya utunzaji wa mazingira imepelekea baadhi ya wananchi
kuvamia katika mapori ya akiba kufanya shughuli za kijamii hali inayopelekea mapori
hayo kukauka kwa vyanzo vya maji na kukosekana kwa mvua.
Kauli
hiyo imetolewa na kaimu meneja wa wakala wa misitu Tanzania wilaya ya Muleba
mkoani Kagera Bw. Samwel Magina wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake.
Bw. Magina amesema kuwa wamekuwa wakiweka doria hususani katika
hifadhi ya Ruhiga ambayo ndio
imeathiriwa na shughuli za binadamu ikiwemo wananchi kukata miti ovyo na
kuchoma mkaa.

Comments
Post a Comment