TANI 6 ZA SAMAKI WACHANGA ZAKAMATWA SENGEREMA.
Takribani tani
6 za samaki
aina ya Sangara
wenye thamani ya shilingi
milioni 24 na nyavu haramu
912 zenye thamani ya shilingi
milioni 22.8 zimekamatwa kwenye
shamba la Bwn,Joseph Kando maarufu
kama Njiwa Pori katika kijiji
cha Kawekamo kata ya Nyampande
Wilayani Sengerema Mkoani
Mwanza.
Akithibitisha kukamatwa
kwa samaki hao kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Mh,Emmanuel Kipole Katibu Tawala wa Wilaya ya Sengerema Bwn,Alen Agustine amesema taarifa za uwepo wa samaki hao
wamepewa na raia wema.
Kwa
upande wake Kaimu Afisa uvuvi wa Halmashauri
ya Sengerema Bwn,
Benedictor Magonda amewaomba wananchi waendelee kutoa ushirikaiano
ili watokomeze uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.
Na
Veronica Martine.






Comments
Post a Comment