MAMLAKA YA HALI YA HEWA YATOA TAHADHARI
Mamlaka
ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa
inayofikia asilimia 80 kuanzia leo Jumatano usiku hadi kesho kutwa.
Taarifa ya TMA iliyotolewa Januari 10, 2018 imesema
mvua hizo zitanyesha katika maeneo mengi ya ukanda wa Pwani ya Kusini ambayo ni
Lindi, Mtwara na maeneo ya Morogoro Kusini.
TMA imetoa tahadhari kwa wakazi wa maeneo yaliyotajwa
kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja na tahadhari
zinazotolewa.


Comments
Post a Comment