DIWANI AWAHAKIKISHIA WANANCHI KUWA ATAIKARABATI BARABARA ITOKAYO IKINA KWENDA MUHAMA B MKOANI GEITA
Diwani wa kata ya
Nyaruyeye Mkoani Geita Mh, Malimi Samson amewahakikishia wakazi wa Vijijiji vya
Muhama B, na Ikina kuwa ataikarabati barabara itokayo Ikina
kwenda Muhama B, hadi Nyarugusu
Mkoani humo.

Kauli ya Diwani
huyo imekuja kufuatia barabara hiyo kuharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha hali ambayo imepelekea baadhi ya akinamama wajawazito kujifungulia
njiani kutokana na vyombo vya moto kushindwa kupita
katika barabara hiyo.
Ubovu wa barabara hiyo umesababisha pia wagonjwa
kuchelewa kufikishwa kwenye matibabu kwa wakati na wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao sokoni kwa ajili ya kujipatia kipato cha kuendesha
familia zao.
Hata hivyo mwaka 2018
ni wakati muafaka
kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi ikiwemo madiwani na wabunge kutekeleza ahadi zao walizowaahidi
wananchi kwani umesalia
mwaka mmoja pekee wa kukamilisha ahadi hizo ili kujijengea imani kwa wananchi.
Na EMMANUEL TWIMANYE
Comments
Post a Comment