AKUTWA AKIWA AMEJINYONGA HUKU CHANZO CHAKE KIKIWA HAKIFAHAMIKI HALMSAHAURI YA BUCHOSA
Mtu mmoja mkazi wa kitongoji cha Nyanzimilile kijiji
cha Nyakabanga kata ya Lugata Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema amekutwa juu ya mti
akiwa amejinyonga hadi kupoteza maisha nje
kidogo ya familia yake huku chanzo cha kifo chake kikiwa hakijafahamika.
Akizungumza
na Radio Sengerema kwa njia ya simu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyakabanga bw Bakari Matugunda amekiri kutokea kwa
tukio hilo huku akimtaja
marehemu huyo kuwa
ni Furahisha Mtabuza mwenyeji wa
kijiji cha Nyakabanga (55)
Bwn,Matugunda
ameongeza kuwa mtu
huyo amepatikana baada
ya wananchi kualikana
na kuanza kumtafuta, ndipo walipomkuta
amejinyonga katika kitongoji
jirani cha Igoma ndani
ya
kata hiyo, hali
iliyozua taharuki kubwa
kwa wananchi.
Katika hatua nyingine Afisa
huyo amedai kuwa
hatua za kuutoa
mwili wa marehemu
bado wanalisubiri jeshi la
polisi kwa uchunguzi zaidi,na kusema kuwa
marehemu ameacha mke na watoto
6.
Na TUMAIN JOHN.

Comments
Post a Comment