WATUMISHI WA AFYA WANAOTOA LUGHA CHAFU KWA WANGOJWA KUKIKONA CHA MOTO WILAYANI SENGEREMA .
Mganga mkuu wa wilaya
ya Sengerema Dkt, Peter Mahu
amewaonya vikali baadhi ya watumishi wa zahanati na vituo vya afya wilayani Sengerema
wanaotoa lugha chafu kwa wagonjwa pindi wanapokwenda kufuata huduma ya matibabu katika vito vyao.
Kauli ya mganga mkuu
imekuja baada ya Radio sengerema hivi karibuni kutembelea
zahanati ya Ngoma A na kupokelewa na malalamiko ya wananchi wa eneo
hilo wakiwatupia lawama waunguzi wa
zahanati hiyo kwa kutoa lugha chafu kwa wagonjwa.
Hata hivyo Dkt, Mahu
amewaomba wananchi kuendelea kutoa
taarifa kwa wahusika pindi wanapokutana na kauli chafu
kwenye
vituo vya afya ama Zahanati ili watumishi hao wachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Said Mahera.
Comments
Post a Comment