UONGOZI WA RADIO SENGEREMA WALAANI VIKALI KUTUMIKA AMBAVYO SIVYO KATIKA JAMII
Uongozi wa Kituo
cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentere umelaani vikali wimbi la waandishi wa habari katika jamii wanaotumia
jina la Radio Sengerema kutafuta habari wakati si waandishi wa habari wa kituo hiki.


Kauli hiyo imetolewa na
Meneja mkuu wa
Radio Sengerema Bwn,Sostenes Tangaro ambapo amesema kuwa
mtu yeyote atakayebainika
kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Hatua ya uongozi wa Radio Sengerema kulaani vikali suala hilo imekuja
baada ya baadhi ya watu kutumia mwavuli wa Radio Sengerema
kutafuta habari katika jamii na
kuwadanganya kuwa ni waandishi wa
habari wa kituo hiki kwa muda mrefu .
Na Emmanuel Twimanye.
Comments
Post a Comment