ZOEZI LA UPIMAJI SHIRIKISHI WA VIWANJA WATARAJIWA KUANZA.
Zoezi
la upimaji shirikishi wa viwanja wilayani Sengerema linatarajia kuanza rasmi
mapema wiki hii katika Kata ya Mwabaluhi
wilayani Sengerema
Akizungumza
na Radio Sengerema baada ya mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa
Kanyamwanza Kata ya Mwabaluhi wilayani Sengerema,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
GEOID GEOMATICS INTEPRISES Bwn Wadson Mwakalila,amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi
hilo.
Hata
hivyo ameongeza kuwa endapo kamati iliyoteuliwa na wananchi pamoja na kampuni
itathibitisha kuwa mmiliki wa kiwanja hana uwezo wa kulipia,kampuni itapima
eneo bila malipo.
Nae
diwani wa Kata ya Mwabaluhi Mh.Alex Kiganga,amesema kuwa zoezi hilo litakuwa na
faida kubwa kwa wananchi na hivyo wajitokeze kwa wingi.
Kwa
upande wao wananchi wameshukuru ujio wa kampuni hiyo na kuwaomba waitishe
mkutano mwingine kwa ajili ya kuwapatia elimu
juu ya jambo hilo.
Na Michael Mgozi.
Comments
Post a Comment