WIMBI LA WATOTO
KWENDA MACHINJIONI KUOKOTA KITOWEO CHA NYAMA NA KUACHA KWENDA
SHULE HATIMAE LATATULIWA WILAYANI
SENGEREMA.
Baada
ya Radio Sengerema kurusha habari inayohusiana na wimbi kubwa la watoto kwenda kuokota
kitoweo cha nyama katika machinjio ya yaliyopo kata ya Nyatukara wilayani Sengerema na
kushindwa kuhudhuria masomo shuleni tatizo hilo limekwisha.
Hayo
yamebainishwa na Mkaguzi wa nyama wilaya ya Sengerema Bwn MORIS NDIHO amesema kupungua
kwa suala hilo ni kutokana na sheria iliyopo kwa hivi sasa ambapo bila leseni
hurusiwi kungia machinjioni.
Hata
hivyo amesema mtu yeyote atakaeingia katika machinjio hayo atachukuliwa hatua
za sheria ikiwa ni pamoja na kulipa faini ya shilling laki mbili ama kifungo
cha miezi sita jela.
Aidha
watu wanaoruhusiwa kuingia katika eneo hilo ni wale ambao wamepima afya zao asiwe
na magonjwa ya kuambukiza kama kifua kikuu ambayo yanaweza kuwa hatarishi
katika kitoweo cha nyama.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment