WAZAZI WATAKIWA KUWASAIDIA WATOTO KUFIKIA NDOTO ZAO ZA KIELIMU SENGEREMA
Wazazi wilayani
Sengerema mkoani Mwanza wametakiwa kuacha kupuuza ndoto za watoto wao
pindi wanapowaelezaa ili kufikia malengo
yao.
Hayo yameelezwa na baadhi ya watoto walipokuwa katika kipindi cha ulimwengu wa watoto
kinachorushwa kupitia Radio Sengerema
ambapo wamedai kuwa wanapenda ndoto zao zitimie ili wafanikiwe katika maisha yao ya baadae.
Nao baadhi ya wazazi wamesema kuwa watoto ni
taifa la kesho hivyo wanatakiwa
kuwasaidia ili wafikie malengo yao.
Sambamba na hayo
wazazi wamewaomba walimu wawe na
ushirikiano kwa wazazi, pamoja na wanafunzi wazingatie wanayofundishwa shuleni
ili waongeze ufaulu wao.
Aidha watoto hao
wamewataka wazazi kuwa ugumu wa maisha
isiwe sababu ya kukwamisha ndoto zao.
Na Glorius Balele.

Comments
Post a Comment