MIGUU KIFUNDO SIO ULEMAVU KWANI UNATIBIKA
Wazazi na walezi
wilayani Sengerema mkoani Mwanza wameombwa
kuwapeleka watoto wenye matatizo ya miguu
kifundo katika vituo vya afya ili wapatiwe
matibabu mapema kwani hali hiyo inatibika.

Hayo yamesemwa na Bwn..Chares Gabriel Mtaalamu Wa Tiba ya
Mazoezi ya Viungo katika hospitali teule ya wilaya ya Sengerema ambapo amesema kuwa ni vyema wazazi
wa watoto wenye matatizo hayo wafike katika matibabu mapema ili watibiwe kwa
wakati.
Mtaalam Gabriel amesema kuwa ni vyema kuzingatia
maelezo ya wataalamu wanayopatiwa ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mazoezi ya mara
kwa mara kwani ni mojawapo ya
matibabu.
Hata hivyo amewataka
wazazi kuwa na mwitikio katika kupata huduma hiyo kwa watoto wenye matatizo ya
miguu kifundo ili waondokanena hali hiyo.
Na Glorius Balele
Comments
Post a Comment