SIKU YA MAADHIMISHO YA WATOTO NJITI DUNIANI
Jamii imetakiwa kufahamu uwepo wa watoto njiti
katika jamii na kwamba inatakiwa kuwathamini na kuwahudumia katika mahitaji yao
muhimu.

Hayo
yamesemwa na Mtaalamu wa kitengo cha watoto njiti Bi.Jesca Mgangara wa
hospital teule ya wilaya ya Sengerema katika
siku ya kilele ya maadhimisho ya mtoto njiti duniani ambapo amesema kuwa
jamii haitakiwi kuwatelekeza wazazi wenye watoto njiti .
Bi .Mgangara
amebainisha sababu zinazopelekea kuzaliwa mtoto njiti ikiwa ni pamoja na magonjwa
kwa mama mjamzito na kufanya kazi ngumu wakati wa ujauzito.
Kwa
upande wao wazazi wenye watoto njiti wamezungumza na Radio Sengerema jinsi
wanavyokabiliwa na changamoto ya kuwalea
watoto njiti kukosa ushirikiano kwa baadhi ya wananchi.
Na Shida Mabula.
Comments
Post a Comment