WASHAURIWA
KUZINGATIA SUALA LA USAFI WA MAZINGIRA.
Wananchi
mkoani dodoma wameshauriwa kuzingatia suala la usafi ili kuepukana na magonjwa
yanayoweza kujitokeza hasa magonjwa ya mlipuko.
Hayo
yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya usafi mtaa wa makongoro manispaa ya
dodoma, bwana Kedmon nyongoto, wakati akizungumza na maisha fm, ikiwa ni katika
kutekeleza rai iliyotolewa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mhe dkt
john pombe magufuli ya kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kufanyika usafi wa
mazingira nchini.
Kwa
upande wake Paul elibariki mbaga ambaye ni mkereketwa wa mazingira amesema kuwa
kwenye mtaa wa makongoro kuna kikundi husika ambacho kinahusika na kukusanya
taka na kuzipeleka sehemu maalumu iliyotengwa na kata kwaajili ya kutupa taka.
Aidha
baadhi ya wananchi wa mtaa wa makongoro wamesema suala la usafi linamuhusu kila
mwananchi hivyo wanatakiwa kuwa na ushirikiano ili kuweka mazingira safi na
kutoa wito kwa serikali kuweka njia mbadala ya matumizi ya mifuko ya nailoni
kwani imeonekana kuwa uchafu kwenye mazingira.
Sambamba
na hayo mwenyekiti wa mtaa wa makongoro amesema wamejiwekea utaratibu wa kulipa
faini ya shilling elfu 50 kwa wale ambao hawatajihusisha na suala la usafi, mtu
huyo atakamatwa na kupelekwa ofisi ya mtendaji kwaajili ya kuwajibishwa.
Comments
Post a Comment