WANANCHI WATAKIWA KUACHANA NA UVUVI HARAMU SENGEREMA
Wananchi wa kijiji cha
kasenyi kata ya Kasenyi wilayani Sengerema wametakiwa kuachana na uvuvi haramu
ili kuyaacha mazalia ya samaki yaongezeke.

Hayo yamesemwa na Afisa
Mtendaji wa kijiji cha kasenyi Bw Juma
Bupamba alipokuwa akiongea na Radio Sengerema
ofisini kwake na kuwataka wananchi wa kijiji hicho kuachana na uvuvi haramu
kwani hali hiyo inapelekea uharibifu wa mazalia ya samaki
Bwn
Bupamba ametawataka wananchi wa kijiji cha Kasenyi kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki ambacho ziwa limefungwa ili samaki waongezekee kwa ajili ya
kupata samaki wa kutosha na wakubwa.
Na Tumain John
Comments
Post a Comment