WANANCHI WA MWANGIKA WILAYANI SENGEREMA WAIOMBA SERIKALI KUCHUNGUZA MCHWA UNAOSHAMBULIA PESA ZA MAENDELEO
Wananchi wa kitongoji
cha Mwangika Senta kilichopo kijiji cha Mwangika katika kata Bangwe Halmashauri ya Buchosa
wilayani Sengerema wameiomba Serikali kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha
zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika kijiji
hicho.
Wakizungumza na Radio
sengerema kwa nyakati tofauti wamesema kuwa mwaka 2015 Mbunge wa jimbo la Buchosa
Dr,Charles John Tizeba ambaye pia ni Waziri wa kilimo, amewahi kukabidhi pampu
ya maji kwa ajiri ya kisima chenye kina kirefu, ilikukabiliana na changamoto ya
maji ambayo imekuwa ikiwakabili wana nchi wa kitongoji hicho
kwa muda mrefu.
Adha ya maji katika kitongoji
mwangika senta imekuwa ikiendelea
kujitokeza huku wananchi wakiwa na sinto fahamu kuhusu fedha ambazo wamechanga
kwa ajili ya kuchimbaji wa kisima tangu
mwaka 2015 walipo changa fedha hizo na
kulaani ukimya wa serikali ya kijiji kushindwa kuwasomea taarifa ya mapato na
matumizi ya fedha hizo.
Radio sengerema imemtafuta
mwenyekiti wa kitongoji hicho lakini jitihada za kumpata hazikufanikiwa, hali
ambayo ikalazimika kumtafuta Mwenyekiti wa kijiji kuzungumzia hali hiyo.
Jumla ya watu miasita
wamena kabiliwa na adha ya maji katika Kitongoji hicho hali ambayo huwalazimu
kufuata huduma hiyo umbali mrefu nyakati za usiku hususani kipindi cha
kiangazi.
Na Katemi Lenatus
Comments
Post a Comment