WALIMU WATUPIANA LAWANA KISA USHIRIKINA

Wananchi wa Kisiwa cha Soswa
halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamewatupia lawama walimu waliojikuta
wamelala nje kwa madai ya imani za kishirikina kuwa ni tukio la kutengenezwa.
Wakizungumza kwenye mkutano wa
hadhara ulioitishwa kwa dharura kujadili suala hilo lililojitokeza usiku wa
kuamkia Novemba 15, mwaka huu, katika viwanja vya shule ya msingi Soswa
wananchi hao wamesema tukio hilo ni la kutengenzwa ili kuishinikiza Serikali
iwape uhamisho kutokana na mazingira magumu wanayoishi.
Mwenyekiti wa kamati ya shule, Lydia Buluba amelaani kitendo hicho
ambacho kinahusishwa na imani za kishirikina huku akiwatupia lawama baadhi ya
walimu waliotengeneza jambo hilo ili wapatiwe uhamisho kwa madai kuwa mazingira
wanayoishi si mazuri.
Walimu waliopatwa na tukio hilo ambapo
kwa sasa wanaendelea kupatiwa matibabu wamesema kuwa wanafanyiwa vitendo vya
kishirikina hata kipindi wanapondwa mawe jamii hiyo haikuamini.
Mkaguzi wa shule wilayani Sengerema,
Elly Msulu aliyefika katika Kisiwa
cha Soswa kwa ajili ya kupata ukweli juu
ya tukio hilo ametaka uchunguzi zaidi ufanyike kujua ukweli wa tukio hilo na
watakaobainika hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa huku akiwaomba
walimu kuwa wavumilivu wakati suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.
Na Veronica Martine
Comments
Post a Comment