WALIMU WANACHANGIA CHOO KIMOJA NA WANAFUNZI.
![]() |
| PICHA KUTOKA MTANDAONI |
Walimu wa shule ya msingi Lugasa
kata ya Nyakaliro Halmashauri ya Buchosa
Wilayani Sengerema Mkoani
Mwanza wamelazimika kuchangia choo
kimoja na wanafunzi wao kutokana na
upungufu wa matundu ya vyoo shuleni
hapo.
Hayo yamebainishwa na
Mwl, mkuu wa Shule ya msingi Lugasa Experansia Malila alipokuwa akizungumza
na Radio Sengerema Ofisini kwake
amesema, shule hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa matundu ya vyoo kwani matundu yaliyopo ni saba na hayawezi kumudu idadi ya wanafunzi hao.
Nao walimu
wa shule hiyo wamesema hawajisikii vizuri kitendo cha kuchangia choo kimoja na wanafunzi wao kwani itapelekea
chanzo cha kuporomoka kwa maadili shuleni hapo.
Kwa upande wao
wanafunzi wa shule ya msingi Lugasa wameiomba jamii na serikali kwa ujumla
iwatazame kwa jicho la tatu ili kuwanusuru na changamoto hiyo.
Aidha Mwl Mkuu wa shule hiyo ameiomba jamii walichukue swala
hili kama tatizo la kwao na siyo Kuiachia
serikali pekee.
Na WINFRIDA NGASSA

Comments
Post a Comment