WALIMU WALALA NJE KWA MIUJIZA WILAYANI SENGEREMA

Walimu saba wanaofundisha Shule ya Msingi
Soswa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema wamejikuta wamelala nje
pamoja na familia zao huku wawili kati yao wakiwa wamenyolewa nywele kichwani
na sehemu za siri.
Mwalimu wa Shule ya Msingi Soswa, Petro Lukas amesema tukio hilo
limetokea usiku wa kuamukia novemba 15 mwaka huu wakati walimu hao walipokuwa wamelala ndani ya
nyumba zao ndipo walipotahamaki usiku wakijikuta wamelala nje.
Amesema asubuhi kulipopambazuka walimu hao wamezinduka
na kutoamini kilichotokea kwani walipoingia ndani ya nyumba zao wamekuta damu
zimetapakaa chumbani na sebuleni pia vibuyu vikiwa vimevalishwa shanga nyeupe
vikiwa kitandani na chini kitendo hicho kimewafanya waombe msaada kwa jamii
inayowazuguka.
Mwalimu Lukas amesema kati ya walimu hao wawili
wameathirika zaidi na tukio hilo kwa kupata mshituko ambapo mmoja amenyolewa
nywele kichwani huku mwingine akinyolewa nywele sehemu za siri.
Kutokana na mshtuko huo mwalimu mmoja amepelekwa
kituo cha afya cha Mwangika kwa matibabu na mwalimu mwingine anaendelea na
matibabu na kwamba hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.
Mganga Mkuu Halmashauri
ya Buchosa, Dk Ernest Chacha amekiri
kumpokea mwalimu mmoja kati yao katika kituo cha afya Mwangika na kwa sasa
anaendelea kupatiwa matibabu na baada ya uchunguzi wa kitaalamu kukamilika
watatoa taarifa.
Comments
Post a Comment