MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI ITAFUTIWE SULUHU YA KUDUMU
Wakulima wa
mtaa wa kilabela
kata ya Mwabaluhi
wilayani Sengerema mkoa
wa Mwanza, wametakiwa kuwa na
ushirikiano na wafugaji
hususani katika msimu
huu wa kilimo
ili kuepuka kutokea
migogoro dhidi ya
wakulima na wafugaji.

Kauli hiyo imetolewa
na mwenyekiti wa
mtaa huo Bwn,
Samweli Macheni Nzungu
ambapo amesema kuwa
kuna wafugaji wanaotaka
kuvuruga amani mtaani
humo kutokana na kutoa
kauli chafu pindi
mifugo yao inapoharibu
mazao ya wakulima.
Bwn, Nzungu
ameeleza kuwa mpaka
sasa amesha pokea
kesi nyingi kutoka
kwa wakulima na
wafugaji na ndani
ya kesi hizo
zipo zilizo tatuliwa bila kufika
ofisini kwake na
mbili zimetatuliwa ofisini
hapo bila kuwa na
shida yoyote kutokana na uelewa
wa baadhi ya
wafugaji.
Aidha Mwenyekiti huyo
amewaomba wakulima na wafugaji
wa mtaa wake
kuachana na malumbano
yasiyo na tija na badala
yake waungane pamoja
ili kupata maendeleo ya mtaa,na
wilaya ya Sengerema
kwa ujumla
Na Thobias Ngubila
Comments
Post a Comment