WAHOFIA KUKUMBWA NA UGONJWA WA KIPINDU PINDU.
Baadhi ya Wananchi
Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza
Wamelalamikia suala la kutozolewa kwa
taka zilizojaa kwenye vizimba kwa muda mrefu
huku Mamalaka husika zikilifumbia
macho suala hilo.
Wakitoa Malalamiko
hayo wananchi
hao wamesema wamekerwa na harufu mbaya
kutoka kwenye vizimba hivyo kwani
uchafu haundolewi kwa wakati huku wakihofia kukumbwa na magonjwa ya
milipuko ikiwemo kipindupindi katika msimu huu wa mvua zinazoendelea kunyesha.
Radio Sengerema
imezulu katika katika viunga
mbalimbali vya mji wa sengerema
ambavyo vinalalamikia kutozolewa
taka kwa wakati ambapo baadhi
ya wananchi wamepasa kilio chao kuwa
licha ya kutozwa ushuru wa taka lakini taka hizo hazizolewi.
Maelezo ya
wananchi yamenifanya
niwatafute wafanyakazi katika kampuni ya
STUMACORT COMPANY LIMITED
ambao pia wamesema
kuwa tatizo la
usafi kutofanyika kwa
wakati ni wao
kutolipwa stahiki yao kwa
muda wa zaidi
ya mwezi mmoja.
Kwa upande
wake Meneja wa kampuni
ya STUMACORT COMPANY
LIMITED Bwn,Charles Ngaiza amekiri
kuwepo kwa deni
la wafanyakazi analodaiwa kiasi cha fedha shilingi milioni 5 laki sita
huku
akiri pia kutozolewa uchafu
uliojaa kwenye vizimba kwa
wakati mwafaka na
kuongeza kuwa ni kwa
sababu ya ofisi yake
kutokuwa makini katika
usimamizi wa ukusanyaji
wa mapato jambo ambalo limepelekea kushindwa kumudu
kulipa stahiki za wafanya usafi.
Sanjari na
hayo Bwn, Ngaiza
ameongeza kuwa kampuni
yake imekuwa kwenye
mkataba na
Halmashauri ya Sengerewma kwa
muda wa miezi mitatu
ambapo mkataba huo umeisha
01.11.2017 , na kwamba
halmashauli imetoa matazamio
ya mwezi mmoja tena kutokana
na kampuni kuonekana
kuwa na changamoto
nyingi ambazo zimekuwa zikiikabili .
Comments
Post a Comment