VIJANA KATA YA KASUNGAMILE WILAYANI SENGEREMA WATAKIWA KUFANYA KAZI
Vijana
wa kata ya
Kasungamile Wilayani Sengerema
Mkoani Mwanza wametakiwa
kulima zao la pamba ili kuongeza
mapato yao kiuchumi na kuacha
kukaa vijiweni katika kipindi hiki cha kilimo.


Hayo
yamebainishwa na Diwani wa kata ya Kasungamile Mh, Julias Mussa Ndekeja wakati akizungumza na Radio Sengerema ofisini
kwake amesema kulima zao la pamba kutawasaidia vijana kuongeza kipato na kupata
mitaji itakayowaendeleza kimaisha.
Mh, Ndekeja ameongeza kuwa hakuna haja ya vijana kuilalamikia Serikali kwa
kukosa fursa za ajira katika kipindi hiki cha masika badala yake wanatakiwa
wajiajiri kupitia kilimo.
Diwani
huyo amewatahadharisha vijana wanaopenda kukaa vijiweni wakati wa kazi waache mara
moja na badala yake wajishughulishe kufanya kazi.
Ameongeza
kuwa ikiwa wananchi pamoja na viongozi watasimamia vyema ufufuaji wa zao la
pamba kuna matumaini makubwa ya zao la pamba kuwa na mavuno mazuri Kutokana na
hali ya hewa inavyoendelea.
Na Charles Sungura
Comments
Post a Comment