UNESCO WALETA MWAROBAINI WA MTOTO WA KIKE KUFIKIA NDOTO ZAKE ZA KIELIMU WILAYANI SENGEREMA.

Mafunzo
yaliyofanyika kwa muda wa
siku nne yaliyolenga
kuutambulisha mradi wa kuwawezesha watoto wa kike kufikia ndoto zao za kielimu yamemalizika Novemba 9 mwaka
huu.
Akifunga
mafunzo hayo mtalaamu wa Elimu
na Afya wa shirika la
umoja wa mataifa linalojishughulisha
na utoaji wa Elimu,Sayansi
na Utamaduni ( UNESCO) Mathias
Hermani amewashukuru
washiriki wote na
kuwaomba wautekeleze mradi
huo kwa nguvu zote kwa
sababu unalenga kuinua maisha
ya mtoto wa kike.
Akizungumza kwa
niaba ya Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya
Sengerema Afisa elimu
wa shule za
sekondari wilayani Sengerema
Godwini Balongo amewashukuru
watumishi wote waliohudhuria semina hiyo
na kuahidi watayafanyia kazi
yale walioelekezwa.
Kwa upande
wake mkuu wa
shule ya sekondari
Ngweli Gibson Dobele ambaye ni mmoja
wa washiriki wa
mafunzo hayo na pia
shule yake ni moja kati
ya shule ambazo
zitafikiwa na mradi
huo amesema endapo
mradi huo utatekelezwa
ipasavyo utasaidia kupunguza
mimba kwa wanafunzi.
Hata hivyo
amesema kuanzishwa kwa
mradi huo kutaongeza
uwezo wa kitaaluma
kwa wanafunzi wa
kike endapo watajitambua.
Na Neema Hussein
Comments
Post a Comment