MVUA YAHARIBU HEKALI 47 ZA MAHINDI NGOMA WILAYANI SENGEREMA
Zaidi ya hekali 47 za mazao ya mahindi katika kata ya Ngoma wilaya ya
Sengerema mkoani Mwaza zimeharibiwa na
mvua ya mawe iliyoambatana na upepo
mkali.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa ugani wa
kata hiyo Bw,STANLEY SHIJA ameiambia radio sengerema kuwa mazao
yaliyoharibiwa ni pamoja na
mahindi mhogo,maharage na mtama.
Ameyataja maeneo
yaliyokubwa na tukio hilo kuwa ni pamoja na kijiji cha Lubungo ,na
Nyabila na kuwaomba wakulima kufanya utaratibu wa
kupanda mazao mapya haraka ili kuendana na msimu wa kilimo.
Hata hivyo amewashauri
wakulima wasisubiri kupata pembejeo kutoka serikalini pekee
kwani watachelewa kwenda na kazi ya msimu wa kilimo
na hivyo wanunue mbegu
kwenye maduka ya
kilimo.
Na Anna Elias

Comments
Post a Comment