MKUU WA WILAYA YA SENGEREMA ATANGAZA VITA KALI KWA VIJANA WASIOFANYAKAZI
![]() |
| EMMANUEL KIPOLE |
Vijana wametakiwa
kufanya kazi kwa bidii ili kujikwamua kiuchumi na kuachana na dhana ya kukaa
vijiweni nyakati za kazi hususani kipindi hiki cha kilimo.
Hayoyamebainishwa na
Mkuu wa wilaya ya Sengerema Mh.Emmanuel Kipole wakati akizungumza na vikundi
vya vijana wilayani sengerema.
Mh.Kipole amesema
kuwa,inasikitisha kuona vijana wakisubili kukimbizana na selikari mitaani
muda wa kazi,jambo ambalo hupelekea
kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu.
Mkuu wa Wilaya amewataka kuutumia ujana wao vizuri pindi wanapokuwa na nguvu,kwani bila kujituma
kipindi cha ujana hawataweza kumudu maisha yao uzeeni, kwani vijana
wanawajibu wa kujenga nchi yao.
Hata hivyo Mh,Kipole ameshangazwa na vijana ambao hawajishugulishi
katika kazi yoyote kwa kuwa wako hatarini
kutumbukia katika makundi ya kihalifu pamoja na utumiaji wa dawa za kulevya,hali ambayo itadidimiza uchumi wanchi kwa ujumla.
Na Michael Mgozi.

Comments
Post a Comment