MELI YAZAMA NA WATU 17 WAOKOLEWA NDANI YA ZIWA VICTORIA
Watu
17 wameokolewa baada ya meli ya MV Julius kuzama ziwa Victoria usiku wa kuamkia
novemba 16 ikiwa na watu pamoja na mizigo, kilomita chache kutoka kisiwa cha
Goziba Wilayani Muleba Mkoani Kagera.
Meli hiyo
inayofanya shughuli zake za usafirishaji kati ya Mwanza na kisiwa cha Gozba
Wilayani Muleba Mkoani Kagera, ilizama ikiwa na nahodha, wabeba
mizigo pamoja na mzigo wa magunia 750 ya dagaa.
Jeshi la
Polisi linaendelea kufuatilia kubaini kama kuna waliosahaulika majini, na
taarifa zaidi zitatolewa baada ya zoezi hilo kukamilika.
Comments
Post a Comment