MATUMAINI YAJA KWA WANANCHI BAADA YA KUANZA KWA UPANUZI WA ZAHANATI KUWA KITUO CHA AFYA
Wananchi wa kitongoji cha Kasenyi ,kijiji cha Kasenyi
kata ya Kasenyi wilayani Sengerema wamekuwa
na matumaini ya mwendelezo mzuri wa upanuzi
wa zahanati ya kijiji hicho kuwa kituo cha afya cha kata hiyo.
Akizugungumza na Radio Sengerema Mwenyekiti wa Kitogoji
cha Kasenyi Bwn, Juma Ramadhan
amesema kuwa upanuzi huo ni agizo la Rais wa awamu ya nne DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE alipoagiza kila kata
iwe na kituo cha afya.
BW RAMADHAN amesema kuwa wananchi wa kata hiyo
wameitikia wito huo na kushiriki kikamilifu katika upanuzi wa zahanati hiyo
kwani kukamilika kwake kutapungunza gharama ya kwenda katika hospitali teule ya
wilaya Sengerema kwa ajili ya matibabu zaidi.
Aidha mwekitikiti huyo amewaomba wananchi wa kijiji
hicho kuendelea kujitolea katika upanuzi wa zahanati hiyo ili waondokane na
adha wanayoipata.
Na Tumain John.
Comments
Post a Comment