MAGUFULI AAIGIZA KUBOMOLEWA KWA JENGO LA SHIRIKA LA KUZALISHA UMEME, TANESCO.
![]() |
| Rais Dkt John Pombe Magufuli |
Katika ziara ya kukagua mradi wa
ujenzi wa barabara katika eneo la Ubungo mjini Dar es salaam,Rais Magufuli
ameagiza sehemu ya jengo ambalo ni makao makuu ya shirika linalozalisha na
kusambaza umeme, TANESCO, kuwekwa alama ya 'X' kuashiria jengo hilo libomelewe.
Jengo jingine ambalo litaathiriwa na
agizo hilo ni jengo la wizara ya maji ambalo lipo jirani.
Imeagizwa majengo hayo kubomolewa
kutokana na kuwa yamejengwa katika sehemu ya hifadhi ya barabara.
Zoezi la bomoa boma limekuwa
likiendelea, ambapo majengo pembezoni ya barabara inayounganisha mji wa Dar es salaam
na maeneo mengine ya nchi yameathirika. Wakaazi wengi waliokuwa wakiishi katika
maeneo yanayodaiwa kuwa katika hifadhi ya barabara wamepoteza makazi yao.

Comments
Post a Comment