KAYA 762 ZAKABILIWA NA UKOSFU WA VYOO GEITA

Jumla
ya kaya 762 zinakabiliwa
na ukosefu wa vyoo
katika
kata ya Bukwimba Wilayani
Nyang’hwale Mkoani Geita .
Awali
akitoa taarifa hiyo mbele ya kikao cha baraza la madiwani Diwani viti maalumu wa kata ya bukwimba Bi. GWIDO TANU amesema
wakazi wa kata hiyo hawana mwamko wa kujenga vyoo vya kudumu hali itakayopelekea mlipuko wa magongwa ya mlipuko hasa katika
kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya Nyang’hwale
Bw,CARLOS GWAMAGOBE amesema wananchi wanatakiwa kujua nyumba ni pamoja na choo
hivyo serikali za vijiji katika kata hiyo wahamasishe ujenzi wa vyoo kwa sababu
magonjwa yakitokea hayatachagua wenye vyoo na wasiokuwa na vyoo.
Aidha
jamii imetakiwa kutambua wajibu wake katika suala la usafi katika mazingira
yanayomzunguka bila kusubiri hadi tamko la serikali.
Comments
Post a Comment