KAMATI YA UPIMAJI WA ARDHI YAPEWA SEMINA
Hatimae
zoezi la utoaji
Semina wa kamati
zilizoteuliwa na wananchi
kwa ajili ya
usimamizi wa upimaji shirikishi wa
viwanja katika kata
ya Mwabaruhi wilayani Sengerema limekamilika.
Semina hiyo
imefanyika katika jengo
la Ofisi ya kata
ya Mwabaruhi kwa
lengo la kuchagua viongozi wa
kamati kutoka mitaa
hiyo miwili ya
Kanyamwanza na Ofisini katika kata hiyo.
Akitoa semina
hiyo Mkurugenzi wa
kampuni ya upimaji
ya Geoip Geomatic
Enterprises
Bwn, Watson Mwakalila
amefungua semina kwa
kuwashukuru wanakamati kwa
mahudhurio yao mazuri na
kuwataka kuchagua viongozi
watatu kwa kila
kamati kutoka kwenye kamati zote
mbili zilizo kuwa kwenye semina
hiyo.
Kwa upande wao wanakamati katika semina hiyo wameonekana kufurahishwa na semina hiyo na kuteua wajumbe watatu kwa kila kamati ambapo kamati ya mtaa wa Kanyamwanza mwenyekiti Revocatusi Marosha,katibu Joseph Max Kayanda na mhasibu ni Oriva John,vilevile kamati ya Ofisini mwenyekiti ni Velitatis Max,katibu Hatari Erasto na mhasibu ni Getruda Nestory.
Aidha
wanakamati hao kupitia
semina hiyo wamewaomba
wananchi kutambua umuhimu
wa hati miliki
na kwamba kupitia hilo sasa wanayofursa
ya kumiliki maeneo
tofauti na ofa
za viwanja zilizokuwa
zikitolewa awali.
Na Thobias Ngubila

Comments
Post a Comment