KAMATA KAMATA YA MIFUGO KUENDELEA NCHI NZIMA

Naibu waziri wa Mifugo
na Uvuvi Abdalah Hamis Ulega amesema
serikali haitasita kukamata mifugo itakayoingia
nchini bila kibali ikitokea nchi jirani.
Naibu waziri ameyasema
hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Ngara mkoani Kagera
Mh,Alex Raphael Gashaza ambapo
alitaka kujua jimbo la Ngara linamifugo mingi ikiwemo ng’ombe pamoja na mbuzi je
ni lini serikali itachimba marambo ya kunyweshea mifugo.
Akajibu swali hilo
naibu waziri amesema wilaya ya Ngara kuwa na Mifugo mingi inasababishwa na
kuingizwa mifugo kutoka nchi jirani bila kufuata utaratibu zilizopo.
Hivi karibuni waziri wa
mifugo na uvuvi LUHAGA MPINA alitangaza kupiga mnada ng’ombe zaidi ya 10,000 wa
nchi za Uganda na Rwanda waliokatwa katika oparesheni inayoendelea nchini.
Na Deborah Maisa
Comments
Post a Comment