HUDUMA YA MAMA WAJAWAZITO NA WATATO YAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA SENGEREMA.
Imeelezwa kuwa Elimu inayotolewa
kwa wananchi juu ya afya ya uzazi pamoja na huduma ya afya kwa watoto walio
chini ya umri wa miaka 5 imewafikia wananchi na kuwa na mafanikio mazuri kwani watoto idadi yao kwa mwezi ni 975 na akina
mama wajawazito ni zaidi ya 200.
Hayo yamebainishwa na
Dkt.NELLSON MTABILWA ambaye ni Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya wilayani
Sengerema wakati akizungumza na Radio Sengerema.
Pia Dkt.MTABILWA
amesisitiza kuwa kutokana na elimu wanayopatiwa ni vyema waendelee kuizingatia
ili kuimarisha afya zaidi na kuepusha vifo kwa watoto wenye umri mdogo na kwa
akina mama wajawazito.
Mganga Mfawidhi
amewaomba wazazi pamoja na walezi wale waliopata elimu juu ya afya ya uzazi
pamoja na huduma ya afya kwa watoto wenye umri mdogo wawe mabalozi kwa wengine.
Na Glorius Balele
Comments
Post a Comment