ELIMU JUU YA UPIMAJI WA VIWANJA SENGEREMA
Wananchi zaidi
ya mia mbili
wamepatiwa elimu juu ya
upimaji wa viwanja katika
mtaa wa kisima cha chumvi
kata ya Nyatukala wilayani
sengerema mkoani mwanza.
Elimu hiyo imetolewa
na mkurugenzi wa kampuni lisilokuwa la kiserikali la upimaji wa
viwanja bwana,WATTSON MWAKALILA
katika
mkutano mkuu uliofanyika
katika eneo la kisima cha chumvi kata ya nyatukala wilayani sengerema.
MWAKALILA amesema kuwa hali
hiyo imekuja kutokana
na tamko la Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli kwa kushirikiana
na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Mh, WILLIMU
LUKUVI kufikia mwaka
2020 Tanzania iwe imetoa
hati kuanzia laki nne
na kuendelea.
Pia amesema
kuwa makampuni takiribani
58 hapa nchini
yameombwa kutembelea halmashauri
na manisipaa na kupanga
bei elekezi ambayo itawasaidia
wananchi kufanikisha
shughuli ya upimaji wa
viwanja.
Kwa upande
wake kaimu mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya
wilaya ya sengerema
Bi, LILIAN KAIZA amesema kuwa
kwa sasa kuna makampuni
manne ambayo yamefika
katika halmashauri ya
wilaya ya sengerema
kwa ajili ya kutoa elimu
hiyo ya upimaji wa viwanja.
Nao baadhi
ya wananchi wamedai
kulipwa fidia endapo
kama mwananchi ataamuliwa
kubomoa nyumba
yake na kupisha
barabara za mitaa
hiyo.
Aidha katika
hatua nyingine B,LILIAN amesema
kuwa hivi karibuni
wananchi wataanza kulipa
kodi za majengo
kwa wenyeviti wa vitongoji
ili kuondoa usumbufu
waliokuwa wakiupata hapo awali ili kuondoa msongamano wa wananchi katika halmashauri hiyo.
Na Enosy Mashiba
Comments
Post a Comment