CHANGAMOTO WANAZOKUMBANA NAZO WAJASILIAMALI WADOGO WADOGO JIJINI MWANZA.
Wajasiriamali mbalimbali
wenye viwanda vidogo vidogo mkoani mwanza wameelezea changamoto mbalimbali
zinazowakwamisha kukuza soko la bidhaa zao ikiwemo ya kutokuwa na uwezo
wa kuthibitishiwa bidhaa zao na TBS pamoja TFDA hali
inayowakwamisha kukuza soko la biashara zao.
Wakizungumza katika
kampeni ya amsha viwanda iliyoandaliwa na shirika la sido kwa
kushirikiana na tiled inayofanyika wilayani nyamagana jijini mwanza wamesema
kuwa wamekuwa wakitengeneza bidhaa zao nzuri lakini wamekuwa hawafikii malengo
kutokana na bidhaa hizo zianakuwa hazijathibitishwa na mamlaka hizo kutokana na
gharama kuwa kubwa ambapo wameiomba serikali kuwasaidia suala hilo
Akizungumzia kampeni hiyo meneja wa sido
mkoani mwanza bakari songwe amesema kuwa lengo la kampeni hiyo ni
kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanachi walioanzisha viwan da vidogo vidogo na
ambao bado ili waweze kufikia malengo na kuendena na tanzania ya viwanda
Aidha msimamizi mkuu wa mradi wa kuwaendeleza
wajasiriamali tanzania tled Frank Jirabi
amesema kuwa kampeni hiyo inatarajia kuwafikia wajasiriamali 1,760 nchi
nzima lengo kubwa ikiwa ni kuwafikia wanawake.
Na Said Mahera
Comments
Post a Comment