ANUSURIKA KIFO KWA AJALI YA PIKIPIKI WILAYANI SENGEREMA
Mtu mmoja
aliyetambulika kwa jina la JEREMIA COSMAS mkazi wa Bukala wilayani Sengerema amenusurika kifo baada
ya kugongana na gari aina ya
probox yenye namba za usajili T 664 DHT katika makutano ya barabara ya Kamanga
na Busisi wilaya Sengerema Mkoani Mwanza.
Ajali hiyo imetokea
baada ya dereva wa pikipiki kuingia katika makutano ya barabara ya kamanga na
busisi akitokea barabara ya misheni na kugonga ubavuni mwa gari lililokuwa likitokea barabara ya Geita.
Mganga mkuu wa
hospitali teule ya wilaya ya Sengerema Dkt.Mary
Jose amethibitisha kupokea majeruhi huyo na hadi Radio Sengerema inaondoka
katika chumba cha dharula hospitalini hapo mgonjwa alikuwa anaendelea na
matibabu.
Jeshi la polisi kitengo
cha usalama barabarani limefika katika eneo la tukio na kuchukua taratibu za
awali kwa mjibu wa sheria.

Comments
Post a Comment