UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Jamii  imetakiwa kutunza mazingira kwa kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo cha kudumu ili kuepusha uharibifu wa mazingira katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na afisa afya wa kata ya Igalula Bwn;Emmanuel Saguda   katika kikao na wananchi wa kijiji cha Nyasigu kata ya Igalula wilayani Sengerema, ambapo amesema kumekuwepo na tabia ya baadhi watu kusubiria ukaguzi ndipo wanatengeneza vyoo vya muda ili kujikinga na ukaguzi huo.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Igalula Mh, Onesmo Mussa Mashiri amewaomba wananchi wote kunzingatia yanayo semwa na wataalamu kwa kutunza mazingira.  

Hata hivyo maeneo mengi  ya vijijini yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya ukataji miti ovyo, uhaba wa vyoo hivyo kupelekea wananchi kujisaidia vichakani jambo ambalo siyo salama kwa afya zao.

Comments

Popular posts from this blog

KISIWA CHA ZILAGULA KIPO HATARINI KUKUMBWA NA KIPINDUPINDU WILAYANI SENGEREMA

WANAFUNZI WAONDOKANA NA ADHA YA KUTEMBEA UMBALI MREFU KUFUATA ELIMU KATIKA KIJIJI CHA ILEKANILO WILAYANI SENGEREMA.