WBUNGE WA UPINZANI WASUSIA KUAPISHWA KWA WABUNGE 7 WA CUF
![]() |
| Baadhi ya wabunge wa upinzani |
Wabunge wa
Kambi ya Upinzani Bungeni wamesusia kuapishwa kwa wabunge saba Viti Maalumu wa
Chama cha Wananchi (CUF) katika mkutano wa nane Bunge la 11 kwa madai
hawakufurahishwa na maamuzi ya kufukuzwa wabunge 8 wa Viti Maalumu wa chama
hicho.
Mkutano wa
nane wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania umeanza leo Mjini Dodoma na
moja ya mambo yaliyopo kwenye ratiba ya mkutano huo ni kuapishwa kwa wabunge
wapya 8 wa Viti Maalumu ambao wameteuliwa kuziba nafasi za wabunge 8 wa Viti
Maalumu waliofutwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba baada ya
kupoteza sifa ya kuwa wabunge.
Wabunge
ambao wamekula kiapo cha uaminifu siku ya leo Septemba 5 ni pamoja
na Alfredina Kaigi, Kiza Mayeye, Nuru Bafadhili, Rukia Kassim,
Shamsia Mtamba, Sonia Magogo na Zainab Amir.
Aidha, CUF
kimewaapisha wabunge saba badala ya nane kama inavyotakiwa kutokana na mbunge
mmoja mteule Hindu Mwenda kufariki siku ya Ijumaa Septemba Mosi
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa upande
mwingine, wabunge wa upinzani waliingia bungeni baada ya wabunge hao
kumaliza kuapishwa na Spika Job Ndugai.
Na Veronica Martine

Comments
Post a Comment