Waziri
Mkuu wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa
amewataka Maafisa watendaji wa mikoa yote nchini kuhakikisha wanafuatilia
maendeleo ya viwanda katika maeneo yao kwani vitasaidia katika kutatua
tatizo la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana.
SULUHU LA UKOSEFU WA AJIRA KWA VIJANA YAPATIKANA

Waziri
Mkuu ameyasema hayo wakati alipozungumza na Maafisa watendaji na wananchi wa
mkoa wa Morogoro ambapo amesema mpango wa Serikali wa kujenga uchumi wa viwanda
ambao unalenga kuinua uchumi wa Taifa kutoka wa chini kwenda uchumi wa kati,
hivyo ni muhimu kuvifuatilia.
Waziri Majaliwa
ameongeza kwamba muda mrefu sekta ya viwanda nchini imekuwa haifanyi vizuri
jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa tatizo la ajira na mazao yalikosa
soko.
Hata hivyo
Waziri Mkuu amesisitiza uaminifu kwa wafanyakazi walioajiriwa katika viwanda
mbalimbali kuwa waaminifu ili kuviwezesha viwanda hivyo kuendelea na
uzalishaji.
Comments
Post a Comment