WAUMIN WA DINI YA
KIISLAMU WOTE WILAYANI SENGEREMA WATAKIWA KUSHEREKEA KWA AMANI NA UTULIVU

Mkuu wa wilaya ya
Sengerema Mh.Emmanuel Kipole leo amewatahadharisha
wazazi kutowaacha watoto wao kutembea wakiwa wenywewe kwenye sikukuu ya Idd
El Hajji.
Akizungumza na radio
sengerema ofisini kwake Mh,Kipole amesema kuwa ameimarisha ulinzi na usalama
huku akiwakikishia kuwa hapatakuwepo na uvunjifu wa amani.
Ameongeza kuwa waislamu
na madhehebu yote wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika kuimarisha amani ya
Tanzania huku akiwaomba kuzidi kutoa maadili
katika jamii.
Aida waisalmu wote
ulimwenguni wanasherekea sikukuu ya Idd
El Hajji baada ya kumaliza hija ambayo hufanyika kila mwaka.
Na Anna Elias
Comments
Post a Comment