WATAKAOIBA MITIHANI
KUBURUZWA MAHAKAMANI
![]() |
| Wanafunzi wa darasa la saba wakitarajiwa kufanya kufanya mtihani |
Jumla ya watahiniwa
Elfu nane mia tano hamsini na
moja wanatarajiwa kufanya mtihani wa
kuhitimu elimu ya msingi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .
Afisa elimu wa shule
za msingi Wilaya
ya Sengerema Bwn,Oscar
Kapinga amebainisha kuwa kati ya
watahiniwa hao wavulana ni elfu
nne mia moja thelathini na nane na wasichana ni elfu nne kumi na tatu .
Akizungumzia suala la usimamizi wa mitihani hiyo Kapinga amesema kuwa wamejipanga vizuri
kuhakikisha suala la udanganyifu wa
kuiba mitihani halitokei huku
akiwatahadharisha wasimamizi na wanafunzi
watakaofanya udanganyifu wa kuiba mitihani hiyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yao.
Hata hivyo afisa elimu amewataka wazazi na
walezi kutowashinikiza watoto wao
kufanya vibaya mtihani hiyo kwa lengo la kushindwa kuendelea na masomo yao ya
sekondari hapo baadae ili wawasaidie kazi za nyumbani pamoja na kuolewa ili wapate mali.
Mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi inatarajiwa kuanza
kufanyika kesho septemba 6 hadi Septemba 7 mwaka huu nchini kote.
Na,Emmanuel Twimanye.

Comments
Post a Comment