WAPIGWA FAINI YA LAKI MOJA KISA LUGHA ZA UCHOCHEZI
| fedha ya Tanzania |
Watu wawili
wakazi wa mtaa wa Nyacheche Road kata ya
Nyatukala Wilayani Sengerema wametozwa faini ya shilingi laki moja (100,000) kwa
kosa la kutoa lugha za uchochezi katika
jeshi la jadi maarufu kama sungusungu.
Hayo yamebainika
kwenye mkutano mkuu wa
sungusungu uliofanyika
katika eneo hilo
baada ya kusomwa
taarifa ya jeshi
hilo na katibu
wa sungusungu Sijali
Ibrahimu.
Baadhi
ya wananchi wamelaani
kitendo hicho na
kusema kuwa ni lazima
wachukuliwe hatua kali
kwani jeshi hilo linafanya kazi usiku
na mchana kuhakikisha
suala la ulizi na usalama linazidi
kuimarika.
Nao viongozi
wa sugusungu waliokumbana
na sakata hilo wametaja
majina ya watu hao ambao wanatuhumiwa
kutoa lugha za uchozhezi.
Nae
mwenyekiti wa kata ya Nyatukala bwn Pelana
Bagume Wametaka wananchi kuachana na lugha za uchochezi kwa zinaweza
kuwasabibishia matatizo makubwa hapo baadae.
Mkutano
huo umehudhuliwa na zaid ya wananchi 181 pamoja na viongozi wa jeshi la jadi
sungusungu kutoka vitongoji kata jirani.
Na Said Mahera
Comments
Post a Comment